Pages

Subscribe:

Monday, April 3, 2017

HUSSEIN MACHOZI: HARMORAPA KIKI ZINAMFUATA ZENYEWE

Msanii Hussein Machozi amefunguka na kusema yeye anampenda na kumkubali sana Harmorapa kwa kuwa anaamini kijana huyu anatafuta maisha na kutoka hivyo yeye anamuombea Mungu ili afanikiwe zaidi.  

Hussein Machozi amesema hayo baada ya baadhi ya watu kuanza kumkejeli na kumsema Harmorapa kuwa anategemea kiki ndiyo maana anasema yeye haamini kama ni msanii wa kiki ila muda mwingine...
hizo kiki zinamtafuta zenyewe.

"Mdogo wangu Harmorapa naye ana simulizi yake ya tofauti kabisa kuhusu namna alivyofika hapo alipo sasa. Ni simulizi ya kufurahisha ambayo nimeona baadhi ya watu wakiikejeli. Mimi kutoka moyoni mwangu, huyu bwana mdogo ananifurahisha sana. Kama kaka yake kwenye muziki namuombea afanikiwe zaidi. Na nadhani hata wenzangu tuliotangulia tunapaswa kumsupport kama tufavyavyo kwa wengine" alisema Hussein Machozi 

Hussein Machozi alizidi kufafanua kuwa
"Siamini kama kijana huyu ni msanii wa kiki, bali nionacho ni kwamba wakati mwingine kiki zinamfuata mwenyewe na anazijua namna ya kwenda nazo. Kila lakheri mdogo wangu, muziki hauna mwenyewe huu, kila mtu mwenye bidii, watu wa kumsaidia, kujituma, zali, baraka za Mungu na vingine anaweza kufanikiwa. Kaza zaidi ili uje kuwa mkombozi wa muhimu kwenye familia yako." alisisitiza Hussein Machozi.

0 comments:

Post a Comment