Pages

Subscribe:

Sunday, April 2, 2017

STORY: NILIFANYA MAPENZI NA MAITI 20 ILI NITAJIRIKE-25

Image result for nilifanya mapenzi na maiti 20 ILI NITAJIRIKE-21
ILIPOISHIA
Kiukweli alinichanganya sana, hapohapo nikamuona akitoka katika sura ya Mudi na kurudi katika sura ya moja ya maiti niliyowahi kufanya nayo mapenzi mochwari, hakika ilinitisha sana. Nikataka nijitoe pale kitandani, akanikandamiza zaidi. Nikahisi kifua kikianza kubana na pumzi kuanza kukata.

SONGA NAYO
Bado macho yangu yalikuwa yakiiona maiti juu yangu, ilikuwa imenikandamiza vilivyo pale nilipolala, sikumuona Mudi kabisa, nilijitahidi kujitoa kutoka hapo kitandani lakini...

nilishindwa.

Nilianza kuhema juujuu, kuna wakati nilihisi kama ningekufa kwani nilibanwa sana kiasi kwamba nguvu zikaanza kuniisha mwilini mwangu. Wakati sura ile ikiendelea kuwa ya hiyo maiti, ghafla ikabadilika na kuwa sura ya Mudi, nilishangaa, hata kule kubanwa kote kukatoka.

“Kuna nini?” aliniuliza Mudi huku akiniangalia usoni.
“Hakuna kitu,” nilijibu huku nikionekana kuwa na hofu kubwa usoni mwangu.
“Hapana! Kutakuwa na tatizo, kuna nini?” aliniuliza Mudi huku akiwa amenikazia macho.


Ni kweli kulikuwa na tatizo lakini sikutaka kumwambia, najua hakuwa akifahamu lolote lile, niliiona maiti lakini kama ningemwambia kuwa nimeiona maiti badala ya kumuona yeye, angenifikiriaje?
Nilijaribu kumwambia kwamba hakukuwa na tatizo lolote lile hivyo angeendelea kama kawaida yake. Tulifanya mapenzi siku hiyo, sikutaka kuondoka, nililala na Mudi hotelini hapo huku usiku mzima nikiota ndoto za ajabu, mara nakimbizwa makaburini na watu waliovalia mashuka meupe, mara nakuchukuliwa na kupelekwa mochwari kisha kuingizwa katika masanduku ya kuhifadhia maiti.


Mpaka tunaamka asubuhi, niliota ndoto mbili, zote zilikuwa za kutisha mno, sikujua kwa nini ilikuwa hivyo, nilitamani nipate majibu juu ya ndoto zile kwamba kwa nini kipindi cha nyuma sikuwa naota ndoto mbaya ila kipindi hicho zilikuwa zikija mfululizo?
Sikutaka kujali japokuwa moyo wangu ulikuwa na hofu kubwa. 


Asubuhi hiyo tukanywa chai na kumwambia Mudi kwamba ningeondoka kuelekea katika kijiji chetu cha Mbingu.

“Ni lazima niondoke mpenzi,” nilimwambia kwa sauti ndogo, ilikuwa kama saa nne asubuhi.

“Sawa! Ila ningependa niendelee kuwa nawe, ila haina jinsi, kwenda kuwaona wazazi ni jambo la msingi sana,” aliniambia kwa unyonge ambao ulinionesha kwamba hata yeye hakupenda kuniona nikiondoka.


Hakukuwa na jinsi, ilikuwa ni lazima niondoke kuendelea na safari yangu. Tulipoagana na kwenda ndani ya gari langu, nikatulia, nikauegemea usukani na kuanza kufikiria kile kilichokuwa kikiendelea katika maisha yangu.


“Tatizo nini tena?’ nilijiuliza lakini sikupata jibu.

Sikutaka kubaki mahali hapo, nikaondoka na kuendelea na safari. Njiani, sikuwa na furaha hata kidogo, wakati nikiwa nimebakiza kilometa kumi kabla ya kufika kijijini, nikashangaa kuona gari likipunguza mwendo kisha kusimama pembezoni mwa barabara.

Nilishangaa, gari hilo halikuwa bovu, kulikuwa na mafuta ya kutosha, sasa kwa nini lilipunguza mwendo na kisha kujizima, nilibaki nikijiuliza sana lakini hata kabla sijapata jibu, niliisikia sauti ya mtu ikiniambia niangalie nyuma kwani kulikuwa na kitu.

Haraka nikayapeleka macho yangu katika siti za nyuma, nilichokiona ni boksi dogo likiwa limefungwa vizuri. Kwanza nikashtuka, sikujua ni nani aliliweka boksi hilo na ndani kulikuwa na nini.

Niliamini hakukuwa na mtu aliyekuwa na uwezo wa kufungua mlango wa gari langu kisha kuingia ndani kwani ufunguo nilikuwa nao, sasa nani alidiriki kuufungua mlango na kuliweka boksi hilo? Nikakosa jibu.

Nikatoka hapo mbele na kuelekea nyuma, boksi lile liliandikwa jina langu kwa juu, nilikuwa na hofu kubwa lakini nilitakiwa kufungua, ilikuwa ni lazima nijue ndani kulikuwa na nini kwa nini lilikuwa ndani ya gari langu.

Wakati nimelichukua boksi hilo, cha kushangaza kabisa mapigo yangu ya moyo yakaanza kudunda kwa nguvu mno, kijasho chembamba kikaanza kunitiririka, sikujua sababu ya kuwa kwenye hali hiyo, kumbuka hapo ilikuwa porini, nilizungukwa na miti kila kona, sikuogopa kuwa hapo, ila hilo boksi ndilo lililonitia hofu.


Nikafungua na kuangalia ndani. Kitu nilichokutana nacho, kilinishtua sana, kulikuwa na kisu kilichofungwa kitambaa chekundu katika mpini wake, nikajiuliza sababu ya kisu hicho kuwa garini mwangu ilikuwa nini?
“Umekiona hicho kisu?” niliisikia sauti ya mganga, niliangalia huku na kule, sikuona mtu, nikashangaa.


“Ndiyo mkuu!”
“Unatakiwa kutoa sadaka moja kila baada ya miezi miwili,” nilimsikia akiniambia.

“Sadaka?”
“Ndiyo! Bado tuna kazi kubwa na wewe, ni lazima ufanye tunachokuagiza ili utajirike zaidi,” aliniambia.


“Tuna?”
“Ndiyo! Sipo peke yangu, mimi na watu wa giza,” aliniambia.
“Watu wa giza?”
“Ndiyo!”
“Akina nani?”
“Waliokupa utajiri,” alinijibu.


Hakika nilishangaa sana, maneno aliyoniambia kama sikuwa nikiyaelewa, ilikuwaje aseme kwamba yeye alishirikiana na watu wengine katika kunipa utajiri na wakati nilichokijua ni kwamba yeye peke yake ndiye aliyenipa utajiri huo?
Nilishangaa sana lakini bado sikuridhika, nilitaka kujua zaidi kuhusu hizo sadaka alizosema kwamba nilitakiwa kuzitoa, zilikuwa sadaka za nini? Fedha au?
“Ni lazima uue?” nilisikia sauti hiyo ikinipa majibu.


“Niue?”
“Ndiyo! Utajiri uliokuwa nao ni utajiri wa damu, huwezi kuwa nao milele mpaka utakapotoa damu, ni lazima uue kila baada ya miezi miwili, hakika utajiri utaongezeka na kuwa mwanamke tajiri kuliko wote nchini Tanzania,” aliniambia.


“Mimi niue?”
“Ndiyo! Hakika hautamfuata mtu na kumuua, angalia tena kwenye boksi,” iliniambia sauti hiyo, haraka nikaangalia, macho yangu yakakutana na kioo.


“Unakiona hicho kioo? Kichukue, kiangalie, unaona nini?” iliniuliza, nikakichukua na kuanza kukiangalia, sikuiona taswira yangu, taswira ambayo niliiona ilikuwa ni ya baba yangu.

“Ichome taswira hiyo kwa hicho kisu,” iliniambia.
“Unasemaje?” niliuliza huku jasho likinitiririka, hakika niliogopa kwani nilijua kwamba endapo ningeichoma taswira ile, basi baba yangu angekufa.

“Ichome…” sauti ya mganga iliniambia, nikabaki nikitetemeka.

0 comments:

Post a Comment