Pages

Subscribe:

Monday, April 3, 2017

EDU BOY AILIPIA VIDEO MOJA MARA MBILI

Msanii wa hip hop Edu Boy amesema video ya ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la 'Naiee' ft Bilnass imemgharimu pesa nyingi tofauti na alivyokuwa amepanga kutokana na mabishano kati yake na director wa video hiyo, Nisha wakiwa 'location'. 

Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Edu Boy alisema ushauri wa kufanya video na Nisha alipewa na kaka yake ambaye alisikiliza wimbo wake na kumuambia kwa ukubwa wa wimbo huo itakuwa nzuri  akifanya video na Nisha lakini alipofika Arusha...
kwa ajili ya ku'kushoot' akajikuta akichelewa 'location' hivyo ikabidi kumlipa Nisha kwa mara ya pili.

"Nilishasikia sifa kwamba Nisha huwa anavimba sana hivyo hata nilipochelewa location ilibidi kufuata mkataba na kumlipa tena baada ya Nisha  kugoma ku'shoot' video yangu". Alisema Edu 

Hata hivyo Edu Boy anakiri kuwa alipoambiwa na kufanya kazi na Nisha alishtuka kwa kuwa anamjua kuwa ni mtu ambaye ukichelewa 'location' anaweza akakurudishia pesa yako lakini kwa kuwa alitamani kufanya video nzuri ilimbidi kukubali. 

Edu Boy aliendelea kusema kwamba video anazofikiria kuzifanya bado hajazifanya ila anajaribu kutengeneza kitu ambacho kitawafurahisha mashabiki zake kwa sasa.

0 comments:

Post a Comment