Pages

Subscribe:

Wednesday, April 5, 2017

MAROMBOSO AFUNGUKA KINACHOFANYA NYIMBO ZA YAMOTO BAND KUVUJA

Ugonjwa wa kuvuja kwa nyimbo ambazo hazijakamilika au muda wake wa kutoka umekuwa ukizidi kukua siku hadi siku na kupelekea wasanii wengine kuwa katika wakati mgumu wa ku-release nyimbo zao tofauti na mipango yao.

Kwa mara kadhaa tumekuwa tukisikia nyimbo za Yamoto Band zikisambaa mitandaoni kabla yakufika kwenye Platform ya Radio. Yaani unashangaa nyimbo inakiki tu mitandaoni lakini...
hujawahi kusikia wao waki-promote kuwa wameachia kazi mpaya. Mfano ni ile nyimbo ya “Kidawa” ya Aslay. Kwa niaba ya Yamoto Band, Maromboso amepiga story na sisi.

Akiongea wiki hii, Maromboso amesema “Inatokea mtu kukuta nyimbo ila sasa sio kuvujisha, Unajua kuna kuvuja nyimbo na kuvujisha. Kuvujisha ni kitendo ambacho kinafanyika makusudi, kuvuja nyimbo nikitu ambacho kinatokea kwa bahati mbaya, ‘either’ kunamistake zimetokea kwa maproducer au kuna mtu alichukua nyimbo akajitia yeye ndiyo yeye akapeleka mjini”. 

Aliongeza, “Kwa hiyo nikisema kuvujisha nikitendo ambacho kimekusudiwa ila kuvuja nikitu ambacho kwa bahati mbaya kwa hiyo nyimbo zetu sisi huwa zinavuja, either kwa sasabu ya production tunayoifanyia kzi inakuwa haina ulinzi mzuri wa nyimbo. Ila mimi ninavyojua tukifanya kitu sisi, tukirekodi kila mtu anakuwa na shauku ya kutaka kusikiliza nini tumefanya, kuchukua labda na kwenda kusikiliza nyumbani  kwa hiyo ilo nalo linachangia mwisho wasiku goma linafika kwenye social network”.

0 comments:

Post a Comment