Pages

Subscribe:

Monday, April 3, 2017

THAMANI YA MBWANA SAMATTA YAPANDA KWENYE SOKO LA WACHEZAJI


Thamani ya Mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania anayekipiga katika timu ya KRC Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta imepanda katika soko la wachezaji duniani. Thamani yake kwa imefikia kiwango cha Euro milioni 3 sawa na shilingi bilioni 7.1 za kitanzania kwa mujibu wa mtandao unaohusika na biashara za wachezaji duniani.

Hatua hiyo imekuja baada ya Samatta kutimiza idadi ya kiwango cha magoli iliyokuwa ikihitajika ambapo ameweza kufunga mabao saba katika mechi sita za hivi karibuni akiwa katika timu yake ya Genk pamoja na...
mawili aliyoyapachika Botswana mchezo uliochezwa na Taifa Stars.

Mabadiliko hayo yamefanyika mwishoni mwa mwezi Machi ambapo mshambuliaji huyo alionekana kung'ara katika ushindi wa bao 4-1 iliyopata klabu yake dhidi ya Lokeren na yeye akitupia bao mojawapo.

Ikumbukwe Samatta alinunuliwa na TP Mazembe akitokea Simba kwa thamani ya Euro 70,000 na kisha kuuzwa Genk kwa Euro 500,000 na sasa timu yoyote ikimuhitaji italazimika kutoa Euro milioni 3.

0 comments:

Post a Comment