Pages

Subscribe:

Sunday, April 2, 2017

RAPPER WA YOUNG MONEY LIL TWIST ATOKA JELA

Baada ya kuchezea ndoo za jela, hatimae sasa karudi uraiani. Mkali huyo kutoka Young Money, Rapper Lil Twist alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kudaiwa kuvunja nyumba ya muigizaji wa zamani wa Nickelodeon, Chris Massey na kuiba Rolex yake na kumpiga mwaka 2014.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Twist amethibitisha kwa sasa tayari yupo uraiani kwa kuandika...
“I’m Home ! Thank God! #YM,”
Akiwa na umri mdogo, rapper huyo alijiunga na Young Money na kuwa na urafiki na Justin Bieber. Maisha yake yalitawaliwa na kashfa nyingi. Mwaka 2013, rapper huyo alikamatwa akiendesha akiwa amelewa gari la Bieber.

Twist ameingia jela Feb. 3 na ameweza kuachiwa huru wiki hii kwa madai yakuonesha tabia nzuri.

0 comments:

Post a Comment