Pages

Subscribe:

Tuesday, April 4, 2017

STORY: SI KITU BILA PENZI LAKO 11

Image result for WALK AWAY
“Au acha. Tutachukua tukirudi” Sauti ilisikika masikioni mwa Patrick.
Mwanaume yule ambaye alitaka kuufungua mlango wa nyuma kwa ajili ya kuchukua vinywaji akauacha mlango ule na kisha kuondoka kuelekea ndani ya eneo lililokuwa kaburi lile. Patrick akaanza kushukuru Mungu, hakuamini kama kweli alikuwa amenusurika kuonwa na mwanaume yule ambaye wala hakuwa amemuona.


Patrick akalifungua shuka na kisha kutoka. Mwili mzima ulikuwa umejaa mavumbi ambayo yalikuwa yakipenya taratibu mpaka mule alipokuwa...

amejifunika kwa shuka. Akaanza kupiga hatua kulekea kule ambako watu walikuwa wakielekea.
Watu zaidi ya elfu tano kutoka katika nchi mbalimbali walikuwa wamekusanyika katika kijiji hicho kwa ajili ya kuangalia kaburi alilozikwa rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere. Wazungu kutoka Marekani, Uingereza na nchi nyingine nyingi walikuwa mahali hapo katika siku hiyo ambayo ilionekana kuwa muhimu katika maisha yao.


Kila mtu alikuwa akimwangalia Patrick ambaye alikuwa mchafu kupitiliza. Walinzi ambao walikuwa wakisimama katika geti la kuingilia eneo la kaburi wakamzuia Patrick. Patrick akaanza kupiga hatua kurudi nyuma hadi kule kulipokuwa na sehemu ya kuegeshea magari na kutulia chini.


Bado kichwa chake kilikuwa kikimfikiria Azizi ambaye hadi kufikia kipindi hicho hakuwa akifahamu sehemu ambayo rafiki yake huyo alipokuwa. Hakuwa na uhakika kama alikuwa hai au alikuwa amekufa baada ya kutoswa majini, kila alipokuwa akifikiria kuhusu Azizi, alikosa raha kabisa.


Masaa yalizidi kusogea huku. Jioni ikaingia, muda ambao watu wakaanza kuingia katika magari yao na kisha kuanza safari ya kuelekea nyumbani kwao na katika hoteli ambazo walikuwa wamepanga. Patrick akasimama kutoka pale alipokuwa na moja kwa moja kupiga hatua kuelekea katika sehemu moja ambayo ilikuwa na magari kadhaa.


Patrick akajaribu kufungua mlango wa buti a gari moja aina ndogo aina ya Chesa mayai. Mlango haukuwa umefungwa kwa ufunguo jambo ambalo lilionekana kumfurahisha Patrick ambaye akaingia ndani kwa haraka haraka na kuufunga.
Zilipita dakika kumi, mara wamiliki wa lile gari wakasikika wakiingia garini na kuliwasha gari lile. Patrick aliendelea kubaki katika buti lile, vumbi likaanza kuingia katika buti lile lililomfanya mara kwa mara kukohoa.


“Thirty kilometres left before we get in Serengeti hotel (Tuna kilometa thelathini hata kabla hatujaingia katika hoteli ya Serengeti)” Mtu mmoja alisikika. Patrick akaisikiliza lafudhi ambayo ilikuwa imetolewa katika uongeaji wa lugha ile, lafudhi ilisikika kuwa ni ya mtu mweusi aliyekulia Afrika.
“Ok! We have to get rooms (Tutatakiwa kuchukua vyuma)” Sauti ya mwanaue mmoja mzungu ilisikika.


Gari liliendeshwa kwa mwendo wa kasi japokuwa barabara haikuwa nzuri. Ndani ya gari hilo kulikuwa na watu wawili, mwanaume mmoja wa kiafrika pamoja na mzungu mmoja. Katika gari jingne ambalo lilikuwa likiongozana na gari hilo, kulikuwa na watu watatu, mwanamke mmoja mzungu, mwanamke mmoja wa kiafrika pamoja na mtoto mmoja wa kike wa kizungu.


Magari yale yalikuwa yakiendelea kukata mbuga mpaka kufika katika hoteli ya Serengeti ambako wakayapaki magari yale na kisha kuanza kuelekea katiika jengo la hoteli ile.


“Jesus Christ! I’ve forgot my laptop. Lydia, go and get me my laptop (Nimesahau laptop yangu. Lydia, kanichukulie laptop yangu) Mwanaume yule mzungu alimwambia binti yake ambaye kwa haraka haraka akarudi katika gari lile.


Akaanza kuitafuta laptop ya baba yake, Bwana Smith lakini hakuweza kuiona. Wazo likamjia kwamba mara kwa mara alikuwa akiiweka katika buti la gari. Akaanza kupiga hatua kulekea katika buti la gari ambako akalifungua na kuingiza mono moja kwa moja bila kuangalia.


Lidya akaonekana kushtuka, akalifungua vizuri boneti lile la gari na kuangalia, macho yake yakakutana na mwili wa mtu, akabaki akitetemeka huku akiuhisi mwili wake kufa ganzi.


Lydia akaanza kipiga kelele huku akikimbia kuelekea katika jengo la hoteli ile. Walinzi wakatokea na kuanza kumfuata Lydia kwa mwendo wa kasi. Mara Bwana Smith ambaye alikuwa kaunta pamoja na wenzake wakaanza kuelekea nje ambako wakakutana na Lydia ambaye bado alikuwa akilia kwa woga.


“Lydia..what has happened? (Lydia...nini kimetokea?)
“A ghost...a ghost...a ghost dad )Mzimu...mzimu...mzimu baba)” Lydia alimwambia baba yake, Bwana Smith
“A ghost? Where is it? (Mzimu? Uko wapi?)” Mzee Smith alimuuliza Lydia
“In the car (Garini)” Lydia alijibu hali iliyowafanya wote kuanza kuelekea garini huku wakiongozana na walinzi.
*****
Hali ya Victoria ilikuwa mbaya kupita kiasi. Kila siku macho yake yalikuwa yamefumba, hakufumbua macho, alitulia kitandani kimya kana kwamba alikuwa amekufa. Udundaji wa moyo wake ndio ambao uliwafanya madaktari na manesi kujua kwamba bado Victoria alikuwa hai.


Mwili wake bado ulikuwa vilevile, micharazo pamoja na alama za mapanga bado zilikuwa zikionekana vizuri japokuwa vidonda vyake vilikuwa vimesafishwa na kupakwa dawa. Victoria aliendelea kubaki kimya kila siku, madaktari na manesi hawakuwa na uhakika kama kuna siku Victoria angefumbua macho na kurudi katika hali yake ya kawaida.


Hakukuwa na mtu ambaye alifika mahali hapo kumuona Victoria, hata wale watu ambao walikuwa wamemleta hospitalini pale hawakuonekana tena. Kila nesi alikuwa akimuonea huruma Victoria ambaye hali yake ilizidi kuwa mbaya.


Madaktari wakafanya kazi ya ziada katika kuhakikisha wanampa Victoria huduma bora. Ndani ya wiki moja, hali yake ikaanza kuonekana kurudi katika hali ya kawaida jambo ambalo lilileta matumaini kwa kila aliyemwangalia.


Tiba iliendelea zaidi na zaidi, Victoria akaonekana kupata nguvu na hata macho yake alikuwa akiyafumbua kama kawaida. Tatizo lilibaki kuwa moja, Victoria hakuwa akiongea. Kila siku alikuwa akiwaangalia manesi ambao walikuja katika chumba chake na kumjulia hali pasipo kuongea chochote kile.


Kila nesi alikuwa akimuonea huruma Victoria ambaye alikuwa ametelekezwa hospitalini hapo. Chakula cha kila siku kilikuwa kikiletwa na wauguzi hao ambao walitokea kumpenda Victoria kuliko mgonjwa yeyote hospitalini hapo.


Miezi miwili ikakatika, Victoria akarudi katika hali yake ya kawaida ambapo akaanza kuwaelezea manesi na madaktari kila kitu ambacho kilikuwa kimetokea katika maisha yake. Kila mtu alionekana kumuonea huruma Victoria ambaye alionekana mdogo sana kupitia matatizo kama yale.


Kila mtu alimshauri kurudi kijijini kwao lakini Victoria hakuonekana kuelewa, hakutaka tena kurudi kijijini. Alimuogopa sana baba yake, hakujua angefanywa nini kama tu angerudi kijijini na kuingia mikononi mwa baba yake ambaye hakuwa na mchezo hata mara moja.


Kwa kuwa Victoria hakuwa na pa kwenda kwa wakati huo, nesi Getrude akaamua kwenda kukaa nae nyumbani mpaka hapo mambo yake binafsi yatakapokuwa salama. Victoria hakuwa na kipingamizi chochote kile, moja kwa moja akaamia nyumbani kwa Getrude ambaye alikuwa amepanga vyumba viwili hapo hapo Nzega.


Kila siku mawazo yake yalikuwa kwa Patrick ambaye hadi wakati huo hakuwa akijua mahali ambapo alipokuwa. Victoria aliumia sana moyoni kila alipokuwa akimfikiria Patrick. Kamwe hakutaka kutengana nae, alikuwa akizidi kumhitaji kila siku.
Victoria alizikumbuka picha zake nyingi ambazo alikuwa akichorwa katika kipindi ambacho alikuwa kijijini. Alimkumbuka Patrick kwa kila kitu katika maisha yake, kwa kifupi, hakutaka kuwa na mwanaume yeyote zaidi ya Patrick.


Kama kawaida, wavulana hawakutaka kuwa nyuma, kila siku walikuwa wakimtaka Victoria ambaye alikuwa akivutia kadri siku zilivyozidi kwenda mbele. Victoria hakuonekana kuwa kushawishika kirahisi, kila siku alikuwa akitunza uaminifu wake kwa Patrick ambaye alimhesabia kuwa mume wake wa baadae.


Getrude akamtafutia Victoria kazi ya kufagia katika ofisi moja ya Usafiri. Victoria alionekana kutisha katika uzuri wake. Watu wengi ambao walikuwa wakifika katika ofisi hizo kwa ajili ya kukata tiketi za kuelekea Dar es Salaam, Mwanza na mikoa mingine, walionekana kuvutiwa sana na Victoria.


Victoria hakuonekana kukubaliana na mvulana yeyote ambaye alikuwa akimwambia kile ambacho kilikuwa moyoni mwake, hakuamini kama kulikuwa na mwanaume ambaye alikuwa akimpenda zaidi ya Patrick. Aliuapiza moyo wake kwamba isingewezekana kwake kumsaliti Patrick japokuwa hakuwa karibu nae.


Bosi wa kampuni hiyo ya mabasi ya Sarafina Transport hakuwa mbali. Fedha zake ndizo zilikuwa fimbo za kuwakamatia wasichana ambao walionekana kumsumbua. Alimjaribu Victoria kwa fedha zake lakini Victoria hauonekana kukubali, bado alikuwa akiitunza ahadi ya kutokumsaliti Patrick.


Msimamo wa Victoria ukamfanya bosi Nhiga kukata tamaa. Hakumfuatilia tena Victoria zaidi ya kuanza kuchunguza ni mvulana gani ambaye alikuwa akimchanganya Victoria mpaka kumkatalia. Kila siku alifanya uchunguzi lakini hakumpata mvulana yeyote yule. Hakuonekana kukata tamaa, bado alikuwa akiendelea na uchunguzi wake.
*****
Maria alionekana kuumia kupita kiasi, maneno ambayo aliambiwa na Hidifonce yalionekana kumuumiza kupita kawaida. Alirudi nyumbani huku machozi yakizidi kumtoka. Maria alionekana kubadilika, kila mtu ambaye alikuwa akimwangalia, alimuonea huruma japokuwa hawakujua ni kitu gani kilikuwa kinaendelea kwa wakati huo.


Maria aliendelea kupiga hatua hadi nyumbani kwao ambapo akaingia ndani ya eneo la nyumba yao. Moja kwa moja akaelekea katika kibaraza cha nyumba yao na kutulia. Maneno ya Hidifonce yalikuwa yakijirudia rudia kichwani mwake, maumivu yaliogezeka zaidi na zaidi.


Ingawa alikuwa hajawahi kutembea na mvulana yeyote lakini jina ‘malaya’ ndilo ambalo lilikuwa likijirudia kichwani mwake. Alijiona kama alikuwa msichana malaya kutokana na kile ambacho alikuwa amekifanya kwa Hidifonce
Alijua kwamba alikuwa na haki zote za kupenda na kuhitaji kwa kuwa alikuwa na moyo wa nyama kama wengine, sasa kwa nini hakupewa nafasi ya kusikilizwa zaidi? Kila alichokuwa akikifikiria mahali hapo, bado alijiona kuumia kupita kiasi, moyo wake ulikuwa katika maumivu makali hata zaidi ya kupigwa na msumari wa moto moyoni.


“Kwa nini hautaki kunielewa Hidifonce? Kwa nini unauumiza moyo wangu namna hii?” Maria alijiuliza lakini alikosa jibu.


Akainuka mahali hapo na kuelekea ndani huku akionekana kuwa mpweke kupita kawaida. Ndani hakukukalika vizuri, kila wakati alikuwa akishika kalamu yake na kuandika jina la Hidifonce kiganjani. Moyo wake ulikuwa katika mapenzi makubwa ambayo hakujua kama kulikuwa na mtu ambaye alikuwa na mapenzi kama aliyokuwa nayo yeye.


Akatamani kumpigia simu Hidifonce lakini hakuwa na namba yake jambo lililomfanya kutulia huku akiiangalia simu yake.
“Naomba uwe wangu Hidifonce.....naomba uwe pamoja nami” Maria alijisemea huku machozi yakianza tena kumlenga.

Je, nini kitaendelea?
***************************************************************************************
Simulizi zitakujia hapa hapa kila siku kuanzia saa tatu asubuhi mpaka saa nne asubuhi na ukipitwa na story basi nenda hapo juu kwenye munyu kisha bofya mahali palipo andikwa LOVE & STORY. Pia waweza kudownload Application yetu kwa kubofya neno DOWNLOAD hapo chini ufuate maelekezo ili uweze kupata story kwa muda muafaka na kwa urahisi zaidi.
 

Tukutane tena kesho muda kama huu.. ahsante

Download


0 comments:

Post a Comment