Pages

Subscribe:

Monday, April 3, 2017

UWEZO WA BILL NASS WAMFANYA JAY MOE ATAMANI KUMWANDIKIA WIMBO

 
Mkongwe wa Hip Hop, Juma Mchopanga ‘Jay Moe’ ambaye anafanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Nisaidie Kushare’ amekiri kutamani kumuandikia mistari pamoja na kufanya kazi na rapa Billnass kama atakuwa tayari, licha ya kumdharau siku za mwanzo.
Rapa huyo amefunguka hayo hivi karibuni na kudai kuwa kabla ya kusikia kazi za Billnass aliwahi kumdharau lakini baada ya kumuona ametamani kufanya naye kazi kwa kuwa amevutiwa na...
uwezo wa rapa huyo anayetamba na ngoma ya Mazoea aliyomshirikiaha Mwana FA.
 
Jay Moe ameongeza kuwa kabla ya kumuona, kusikiliza na kutazama video zake hakuwa akijua uwezo mkubwa alionao rapa huyo hivyo hata alipotumiwa wimbo wa rapa huyo na meneja wake alidharau hakuusikiliza hadi walipokutana nchini Afrika Kusini.

“Unajua kuna siku meneja wake, Billnas ‘Mchafu’, alinitumia wimbo akiniomba niwatumie na wengine lakini mimi sikufanya hivyo, nilipowakuta Afrika Kusini na kuwahoji wakaniambia wapo kwa ajili ya kufanya video ya wimbo alionitumia, nilijisikia vibaya sana na niliona aibu maana niliona video yake ni kali tofauti na nilivyokuwa nikimdhania,” Jay Moe alifunguka

Mkongwe huyo amesema alijifunza kitu kupitia Billnass na kwamba hupaswi kumdharau mtu usiyemfahamu.
"Hapo nikajifunza kitu kuwa hutakiwi kumdharau mtu, maana dogo ana uwezo mkubwa wa kurap na anajua nini anafanya hadi nimemwahidi kufanya naye kazi,”  alisema Jay Moe.

0 comments:

Post a Comment