Pages

Subscribe:

Wednesday, April 5, 2017

KAULI YA JOH MAKINI JUU YA VIDEO YAKE ANAYO SHOOT NA DAVIDO


Usiku wa kuamkia April 4 tulikutana na post ya Davido katika kurasa yake ya Instagram akionyesha kinachoendelea pande za S.A akiwa na Mtanzania Joh Makini wakishoot video ya ngoma ambayo ameshirikishwa na Joh.

Post ambayo ilimake headlines na kumaliza maswali ya wapenzi wengi wa muziki wa Joh Makini kuhusu ile collabo ambayo walikuwa wakiiisubiri kwa muda mrefu ya Joh Makini na mkali huyo kutoka Nigeria. Mwandishi aliamua kumtafuta Joh Makini na kupiga naye story kuhusiana na kilichokuwa kikitrend katika mitandao, na Joh hakusita kufunguka...
kila kitu kuhusiana na kilichokuwa kikiwachelewesha wawili hao katika kuikamilisha collabo hiyo na kuiachia.

“Huu wimbo haukutoka mapema zaidi kwasababu tulipokuwa tumeurekodi hatukupanga tuutoa kwa haraka hiyo, tulipourekodi tulisema siku tukipata time tutafanya video ndio tuutoe, kwahiyo tukawa na u-busy hapa kati, mimi nikawa busy na projects za Joh Makini na Weusi na yeye akawa busy na biashara zake”. Alisema Jo Makini.

Pia Joh aliongeza kuwa “Huwezi kulazimisha kitu na mara nyingi vitu kama hivi ukilazimisha unaweza ukaharibu, kwasababu muziki wenyewe ambao tumeutengeneza sisi sio muziki wa kupitwa na wakati, hakuna mtu ambaye alikuwa na stress kwa suala la huu wimbo kuwa ndani.”

0 comments:

Post a Comment