Pages

Subscribe:

Friday, April 7, 2017

NAPE AMLILIA ROMA, ASEMA HAYA

Ikiwa leo ni siku ya pili tangu ilipotolewa taarifa kuwa msanii Roma, Moni Centrozone, producer wa Tongwe Records, Bin Laden na vijana wengine waliotekwa na watu wasiojulikana walipokuwa katika studio hizo, bado haijafamika walipo.

Hata hivyo Jitihada za awali zilizofanywa na watu wao wa karibu, akiwemo mke wa Roma, Nancy zimegonga mwamba. Katika mahojiano na vyombo mbalimbali vya habari wiki hii, Nancy alisema...
nimezunguka katika vituo vingi vikubwa vya polisi kuulizia taarifa za mumewe jibu analokutana nalo ni ‘hatuna taarifa zozote, tutashughulikia.’

Waziri wa zamani wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amemlilia msanii huyo. Nape ametoa kilio chake kupitia ukurasa wake wa Twitter, akitumia maneno matatu pekee yanayosomeka kwa hisia za ndani kuwa ni mtu anayemlilia mpendwa wake. “Roma! Oooooh No!” ametweet Nape.
(Tweet)
Mbunge huyo wa Mtama ameongeza nguvu kwa kilio cha wadau wa muziki pamoja na wasanii waliotumia mitandao ya kijamii kushinikiza ifahamike alipo msanii huyo na wenzake.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa jana na uongozi wa Tongwe Records, watekaji walifika katika studio hizo na kuwahoji waliokuwepo, kisha kuondoka nao wote pamoja na baadhi ya vifaa vinavyotumika kurekodia muziki, kwenda kusikojulikana.

Leo mchana, wasanii wamekutana katika studio za Tongwe Records kwa lengo la kuzungumzia suala hilo zito ambalo limevunja mioyo ya wadau wa muziki, familia na ndugu wa Roma na wenzake.

0 comments:

Post a Comment