Pages

Subscribe:

Thursday, April 6, 2017

STUDIO YA TONGWE YAVAMIWA NA WATU WASIO JULIKANA, ROMA NA MONI WABEBWA NA MAJAMBAZI


Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule aka Professor Jay, amesema rapper Roma Mkatoliki pamoja na rapper Moni Central Zone wamechukuliwa na kupelekwa kusikojulikana na watu waliozivamia studio za Tongwe Records jana usiku.
Profesa amedai watu hao wamemchukua pia kijana wa kazi, computer ya studio pamoja na TV.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Profesa alitoa taarifa hii kwa kuandika:
“ROMA MKATOLIKI AMEKAMATWA USIKU HUU… Nimestushwa sana kusikia kuwa kuna watu wamevamia studio za TONGWE RECORDS majira ya saa...
moja usiku na wamemchukua ROMA @roma2030 , MONI @moni_centrozone na kijana wa Kazi na pia wamechukua COMPUTER ya studio na Screen (Tv) na wameondoka navyo kusikojulikana.. Mpaka sasa hatujui wamewapeleka wapi!!”

0 comments:

Post a Comment