Pages

Subscribe:

Wednesday, April 5, 2017

LINAH: WAZAZI WALIMKATAA MWANAUME ALIYENIPA UJAUZITO


Msanii wa muziki Linah Sanga ambaye kwa sasa ni mjamzito amefunguka kwa kudai kuwa wazazi wake walimkataa mpenzi wake wa sasa kwa kigezo cha dini. Muimbaji huyo ambaye amelelewa katika misingi ya dini ya kikristo, amekiambia kipindi cha XXL cha Clouds Fm kuwa haikuwa rahisi kwa wazazi wake kumkubali mwanaume huyo.

“Mwanzoni wazazi wangu walimkataa mpenzi wangu kisa ni dini tofauti na mimi, lakini sasa hawana pingamizi,” alisema Linah. “Tumeunganisha damu na kwenye mahusiano naamini...
upendo, nisingependa mtu anipangie, lakini jambo la wazazi kwa familia za kiafrika ni tofauti,”

Aliongeza, “Nimebeba ujauzito katika right time kwangu na mwenzangu yupo tayari. Mashabiki wategemee ndoa kabisa muda wowote.” 

Muimbaji huyo kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Mfupi’ aliouachia hivi karibuni.

0 comments:

Post a Comment