Pages

Subscribe:

Wednesday, April 5, 2017

RAYVANNY: NILIKUWA NAFIKIRIA NTAIMBA AINA GANI YA WIMBO NA BAHATI


Baada ya msanii wa muziki wa WCB, Rayvanny kushirikiana na msanii wa Injili wa Kenya, Bahati katika wimbo ‘Nikumbushe’ amefunguka kuzungumzia namna alivyoweza kushirikiana kimuziki na muimbaji huyo wa Injili na kuweza kupata kitu kizuri.

Akiongea katika kipindi cha Jahazi cha Clouds FM Jumanne hii, Rayvanny amedai kabla ya kuanza kuimba alianza kuimba kwaya kanisani. “Kwanza mimi nimekuwa nikimfuatilia Bahati kwa muda mrefu na nilikuwa...
nikifikiria nikikutana naye nitaimba wimbo wa aina gani na mimi niliwa narap huko nyuma lakini nimejua kuimba kwa kupitia kanisani. Kwa hiyo haikuwa ngumu kwangu kufanya kwa sababu ni wimbo wakijamii zaidi ndio maana wimbo hauonyeshi kama ni wa Injili au wakidunia,” alisema Rayvanny. 

Video ya wimbo huo imeachiwa Jumanne hii mtandaoni huku audio ukipatikana katika mtandao wa Wasafi.Com.

0 comments:

Post a Comment