Pages

Subscribe:

Tuesday, April 4, 2017

BARNABA AKIRI UWEPO WA MUNGU BAADA YA KUTOKEWA NA MUUJIZA SIKU YA LEO

Siku kadhaa baada ya kutoa taarifa ya kuibiwa vitu katika gari yake ikiwemo pasi ya kusafiria msanii wa kizazi kipya Barnaba 'Baba Steve' amewataka watu waamini Mungu yupo baada ya asubuhi ya leo kuletewa vitu vyake kwenye bahasha. 

Hit maker huyo wa ‘Lover Boy’ amesema kuwa Mungu amemtendea miujiza baada ya kijana aliyejitambulisha kwa jina moja la...
John kumpatia bahasha iliyokuwa imetupwa ikiwa na vitu vyote muhimu alivyokuwa ameibiwa.

“Amini msiamini Mungu yupo na ukitembea na Yesu hakuna linaloshindikana vitu vingine vimekosekana lakini hivi ni vikubwa zaidi nawashukuru wote mliopambana na kuniombea asante sana baba paroko kwa maombi mazito jana yametenda miujiza” aliandika Barnaba.

Kutoa pesa katika vitu ambavyo vilikuwa vimeibiwa ni pamoja na kitabu cha chuo kidogo cha sala ambapo msanii huyo amesema ni kitabu anachokitumia mara kwa mara anapofanya ibada zake.

“Na hiki kitabu huwa nakitumia sana kwenye ibada zangu za kila kukikucha hasa kwenye sala ya asubuhi jioni usiku pia na moja ya ulinzi wangu nacho kilikuwemo humo Mungu ametenda miujiza” Barnaba aliongeza
Baadhi ya vitu vilivyokuwa vimeibiwa, na sasa vimepatikana

0 comments:

Post a Comment