Pages

Subscribe:

Monday, April 3, 2017

DRAKE AUMIZA KWENYE BILLBOARD 200


Kwa harakaharaka jina la utani ambalo tungempatia Drake kwa sasa na Album yake ya “Moe Life” tungemuita Halichachi tu kwa sababu kila siku, wiki anazidi kufanya vizuri.

Baada ya kfanya vizuri kwenye mitandao ya kustream nyimbo kwa kuwa na wasikilizaji wengi zaidi, Drake ameingia kwenye rekodi nyingine ya kukaa nafasi ya kwanza kwenye  Billboard 200 albums, na chati hiyo imetokana baada ya kuuza kopi ya project yake takribani...
225,000 kwa wiki yake ya pili yangu kuachiwa kwake.

More Life ya Drake inakuwa ni Album ya pili kwa Drake kwa kufanikiwa kushika nafasi hiyo kwenye chati hizo kubwa ambapo Album ya Views ilifanikiwa kukaa kwa takribani Wiki 13 kwenye chati hizo, kwa ujumla sasa Drake anajumla ya wiki 20 kwa album zake kuingia kwenye Billboard 200 ambapo msanii wa kwanza wa HipHop kuwa na wiki nyingi kwenye Bllboard 200 ni Jay z akiwa na wiki 23 alafu akifuatiwa na Mc Hammer akiwa na wiki 21.

0 comments:

Post a Comment