Pages

Subscribe:

Monday, April 3, 2017

NAY WA MITEGO: USALAMA WA MAISHA YANGU NI MDOGO KWA SASA

Msanii wa muziki wa hip hop ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Wapo’ Nay wa Mitego ametangaza hali isiyo kuwa ya kawaida hususani juu usalama wa maisha yake kwa kile alichosema kuwa anaviziwa auwawe na watu wasiojulikana huku chanzo kikiwa bado hajakiweka wazi moja kwa moja.

Wiki moja iliyopita rapper huyo alikamatwa na jeshi la polisi kutokana na wimbo wake mpya ‘Wapo’. Hata hivyo Rais Magufuli alitoa tamko la kuachiwa kwa msanii huyo na kusema wimbo huo hauna matatizo. Leo kupitia...
ukurasa wake wa Instagram amefunguka kwa kudai kuwa kuna watu wanamfuatilia kutaka kumpoteza.
“Usalama wa maisha yangu umekua mdogo kwasasa, Wanapanga kunipoteza ikibidi nisiwepo kabisa kwenye hii dunia.,” aliandika Nay wa Mitego Istagram.

Aliongeza, “Nipo tayari kwa chochote wanacho panga kufanya Coz sijajipanga kupambana nao, Mimi ni mwana muziki si vingine. Kwa chochote kitachotokea familia yangu itakua na chakuongea. Siwezi kuhama nchi wala kukimbia nitafia hapa hapa. Na siko tayari kupindisha chochote.! nyie Ndo mtanilinda. Sina Mlinzi na sitarajii kua na mlinzi. OnlyGod#Wapo,”

Rapper huyo hakuweka wazi ni nani anataka kufanya hivyo.

0 comments:

Post a Comment